Diamond ataja fedha anazolipa kwenye kolabo za Marekani

Diamond amefunguka kuhusu fedha anazowalipa wasanii wa Marekani kwa ajili ya kufanya kolabo.


Diamond Platnumz
Akiongea na Dizzim Online hit maker huyo wa Hallelujah amesema kuwa hakuna fedha yoyote ambayo amewahi kumlipa msanii yoyote wa nchi hiyo ambao tayari ameshafanya nao kolabo.
“Mimi sijawahi kulipa kolabo yoyote kwanza ya Marekani niliyowahi kufanya, sijawahi kulipa na ukichunguza kiundani kolabo zangu na Wamarekani siyo kitu ambacho ‘nimejishobokesha’ ni watu wenyewe ambao wanatokea kunikubali na kuupenda muziki ambao ninaufanya,” amesema Diamond.
Msanii huyo ameongeza, “Ndio maana unaona sometimes sipost naona kama sina haja ya kupost ikiwa wao wenyewe wanakuwa wanafurahi na wanapenda kupost kitu tunachokifanya. Sometimes naogopa kupost naonekana kama nitajishauwa, sitaki kuonekana hivyo, nataka nionekane pointi yangu kuuchukua muziki wa Tanzania kuupeleka mbali.”