Alikiba kuliamsha dude muda wowote.

Ni kweli Alikiba anampango wa kuachia ngoma mpya hivi karibuni?


Huenda jibu likawa ni ndio kutokana na picha mbili ambazo amezipost kupitia mtandao wake wa Instagram na ujumbe ambao ameuandika kwenye picha hizo.
Msanii huyo ambaye aliachia ngoma yake ya ‘Seduce Me’ zaidi ya miezi miwili iliyopita, amepost picha ya kwanza kwenye mtandao huo akiwa peke yake na kuandika, “What Next …? #KingKiba.”

Kiba hakuishia hapo, baada ya muda mfupi kupita aliweka picha nyingine akiwa na director maarufu Afrika, Meji Alabi kitu ambacho kinaonyesha kuwa kuna kila dalili kama ngoma hiyo inakuja basi tutarajie kuona kichupa kilichoongozwa na director huyo wa Nigeria ambaye amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu zaidi na Rockstar4000.