Shilole amfungukia Barakah The Prince, ‘ana dharau sana yule mtoto’

Baada ya Barakah The Prince kumuhusisha Shilole katika kile anachodai kufanyiwa mchezo mchafu katika YouTube channel yake, hatimaye Shilole amejibu.
Barakah alimshtumu Mx Carter kuwa ndiye anafanya mchezo mchafu katika YouTube yake na taarifa hizo alipatiwa na Shilole kitu ambacho kimekanushwa.
Shilole amesema Barakah anataka kumgombanisha na Mx ambaye amekuwa akimsaidia katika mambo mengi ikiwemo kurudisha page yake ya Instagram ambayo ilidukuliwa.
“Lakini kwanini huyo mtoto anapenda kugombanisha watu ndio maana haelewani na watu kwa sababu ya mambo yake anayoyafanya siyo vizuri kama unataka kuongea na mtu mfuate binafsi si mpaka upitie kwa mtu mwingine” amesema.
“Sikipendi nasema ukweli halafu yule ni mdogo wangu namuheshimu, yule mtoto ajipange tunajua sometime unataka kiki lakini siyo za namna hiyo, ana dharau sana yule mtoto, ninasema haitampeleka popote, mimi kwangu hatapata kiki bali nitamuharibia, sitoe kiki kishenzi” Shilole amesisitiza.
Shilole ameongeza kuwa hajawahi kuongea na Barakah jambo kama hilo na mara ya mwisho waliongea kwenye simu ambapo Barakah alimuomba amsaidie kumpostia wimbo wake.
Source; Bongo5