Utakuwa uongo kusema nimefika level ya Alikiba na Diamond – Aslay

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Aslay amesema si sawa kulinganishwa na wasanii wakubwa mfano wa Alikiba na Diamond.Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Natamba’ amesema anaona bado kuna kazi anapaswa kufanya ili kuwafikia wasanii na watu wanaomlinganisha na hao watamfanya abweteke.
“Kwanza mimi huwa sipendi kufanishwa na wasanii wakubwa, kwa sababu kwanza ukinifanisha unanifanya akili yangu ilale, halafu mimi mwenyewe najiona sijafika sehemu fulani” Aslay ameiambia EATV.
“Na hata meneja wangu na watu wanaonizunguka wanaweza kusema wewe bado hujafika sehemu aliyofika labda Alikiba au Diamond, huo utakuwa uongo kusema eti Aslay kafika level ya Alikiba na Diamond au msanii yeyote ambaye ameshavuka mipaka ya nchi na kupeleka muziki na watu wakampenda, bado sijafikia hatua hiyo” amesisitiza.